About Hannah Lalimbo Mgharo

KUZALIWA

Marehemu Hannah Lalimbo Mgharo ni mtoto wa sita katika familia ya marehemu Bwana Josiah Mgharo na
marehemu Bibi Mariam Ndawa. Marehemu alizaliwa mwaka wa 1962, Kijiji cha Silalonyi-Kishamba, Taita-
Taveta. Marehemu ana ndugu ambao ni, RahelMachocho, Margaret Kululo, Joyce Mkami, marehemu
AShton Mtuweta, marehemu Noel Mgharo na marehemu Samuel Mengo.

MASOMO
Marehemu Hannah Lalimbo Mgharo alianza shule ya chekechea Mambura, akasoma mwaka mmoja. Baada ya chekechea, alienda shule ya msingi ya Kikambala miaka saba. Alitangulia na kujiunga na shulee ya upili ya Murray Girls kidato cha kwanza hadi cha nne, na kisha kujiunga na kidato cha tano na cha sita katika shule ya Coast Girls. Mwisho alijiunga na shulee ya mafunzo ya kitalii, Utalii College.

KAZI
Marehemu Hannah Lalimbo Mgharo alijiunga na wizara ya huduma za jamii (social services) huko Kabarnet. Baadaye alijiunga na chuo kikuu cha Egerton Njoro mjini Nakuru hadi mwaka wa 2011, ndipo alipohamia ulaya, Scottland kujiunga na hoteli kisha hospitali.

NDOA
Marehemu Hannah Lalimbo Mgharo alijaliwa na ndoa mwaka wa 1990. Akabarikiwa kupata mtoto mmoja wa kiume ambaye ni AlbertoMtuweta. Alijaliwa na mkaza mwana mmoja ambaye ni Jackline Tangai
na mjukuu mmoja ambaye ni Hannah Tiara Mtuweta. Marehemu Hannah Lalimbo Mgharo alikuwa mkristo
na kubatizwa katika kanisa la Anglikana la ACK St.Stephen Mwakinyungu.Baadaye alijiunga na kanisa la
Amazing Word Kikambala pamoja na familia yake, kanisa linaloongozwa na mchungaji Alex Julius
Kazungu.

MAISHA YA IMANI
Marehemu Hannah Lalimbo Mgharo alianza kulalamika kwa maumivu ya mgongo ikafata miguu
na tumbo mwaka wa 2023. Alipopelekwa hospitali, akigundulika kuwa anaugua saratani ya umio mwaka 2024 mwezi wa Februari. Alipoona hali yake imezidi kuwa mbaya, aliamua kurudinyumbani kwa mtoto wake mwaka 2024 mwezi Mei.Ilipofika tarehe 9 Januari mwaka wa 2025, hali yake ilizidi kuwa mbaya na kukimbizwa katika hospitali ya Mombasa na hapo ndipo alipoaga dunia.Neno lake la mwisho kwa aliowaacha lilikuwa ni, “mbakina amani”.

Mungu alitupa na Mungu amechukua.Jina lake na libarikiwe, Amen!!!

Funeral Details

  • Thursday, January 9th, 2025
    12:00 am
Get Direction

Write memory

  • Rating
Choose Image
Choose Video